October 06, 2010

Wizi Wa Kazi Kuendelea Kumuweka Jela Lil Wayne:

Wakati siku za kutoka jela kwa CEO wa Cash Money Lil Wayne zikiwa zinapiga hodi kumeibuka mengine makubwa kabisa ambayo huenda yakamsababishia mkali huyo kuendelea kusubiri
kwanza kabla ya kutoka

Mashaka ya kisheria juu ya Lil Wayne yamejitokeza tena baada ya mahakama inayosikiliza kesi yake kudai kuwqa jamaa huyo pia anashutumiwa kwa makosa ya kuvunja haki miliki za umiliki wa Wimbo

Ukikubali jicho lako likutupie katika magazeti mbalimbali ya marekani ya leo utakutana na Info inayomuhusu jamaa huyo akidaiwa kushindwa kutimiza makubaliano na producer Mali Boi aliedai kuwa Wimbo wa "Mrs. Officer,"ulikuwa ni wa kwake lakini alikubaliana na Lil Wayne kuurudia lakini ikjiwa ni kwa makubalino maalum

Michael Bradford a.k.a Mali Boi, amesema katika wiumbo huo ambao LilWayne amemshirikisha Bobby Vallentino amesema kuwa Mwaka 2003 alitengeneza wimbo huo ambao Wizz alitumia baadhi ya Vionjo katika wimbo wake wa Mrs Officer

Kutokana na hali hio huenda sasa Lil Wayne akaendelea kuwepo kwa Side Mwema hata Baada ya tarehe yake iliopangwa ya kutoka NOV 13 ikapita

COMMENTS

Inavyoonekana jamaa anayatamani mauzo yaliotokana na wimbo huo uliofanikiwa kuuza zaidi ya nakala Millioni 3 marekani pekee

No comments:

Post a Comment