October 07, 2010

Just Blaze Ajitetea Kuchelewa Kwa Albamu Mpya Ya T.I

Kuchelewa Kutoka kwa Albmu mpya ya T.I na Jay Electronica kumonekana kuwashangaza wengi na kumlazimu mtayarishaji wa Albamu hizo Just Blaze kuamua kufunguka na kuweka wazi sababu za kuchelewa huko. Awali ilitangazwa kuwa Sept 28 kuwa Albamu hizo ndio zingeingia  sokoni lakini kutokana na matatizo ya kisheria ikiwemo kesi iliokuwa ikimkabili T.I imelazimu Albamu hizo kuchelewa kuingia Sokoni

T.I alitazamiwa Kutoa Albamu yake mpya ya "King Uncaged"nae Jay Electronica alikuwa akitarajiwa kutoa Albamu mpya ya "Act II."lakini mpaka sasa Albamu hizo hazijatoka

Producer huyo ambae pia alishiriki katika utayarishaji wa Albamu ya JAY Z Blueprint 3 ameongeza kuwa kuchelewa kwa Albamu ya JAY kulitokana na kuhisi kuwa Ubora wa Albamu hiyo ulikuwa bado haujafikiwa kiwango kinachotarajiwa na mafans wa T.I, So kama angewazingua mashabiki wake

Lakini Just Blazy amehakikisha kuwa Albamu hizo mbili zitakuwa kwa Hewa mapema iwezekanavyo huku akiahidi kuwa mpaka kufikia sasa karibu nyimbo takribani 70 zimesharekodiwa kutoka katika Albamu hizo

No comments:

Post a Comment