October 07, 2010

Chelsea Handler Akana Kuwa Na Mahusiano Ya Chumbani Na Mkali Wa Mabifu 50 Cent:

 
Vyombo vya habari hasa Internet zimekuwa busy sana kwa wiki nzima sasa wakati picha za mwanadasexy independent diva Chelsea Handler na Sent Hamsini a.k.a Curtis Jackson a.k.a Fitty Cent zilipozagaa katika mitandao kwa uvumi kwamba wawili hao wana mahusiano ya kikubwa zaidi.

Hata hivyo bishost huyu wa kishua zaidi kimkwanja ameandika katika Account yake kwenye mtandao wa Twitter kupitia (@chelseahandler) na kueleza kuwa hakuna kilicho nyuma yake na rapper huyo anayeongoza kwa kuwa na mpunga wa kutosha kupita wanamuziki wa kiume wote duniani, zaidiya masuala ya kibiashara tu nasio vinginevyo.

"Sikilizeni Jamani, Nilikutana na Mr. Cent kwa ajili ya masula ya kikazi tu, Hakuna cha kuwaeleza kwa sasa kuhusu mipango yetu lakini mambo yakiwa poa nitawajulisha kama kuna ishu zaidi ya biashara. Chelsea aliandika kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter Jana Oct 6.

Wakati kwa Upande wa Mr. Beef 5O Cent alipokuwa akiwahojiwa na mapaparazi kuhusu uvumi wa mahusiano yake na Chelsea, Fitty Hakua Na Jibu Zaidi ya kutabasamu tu muda wote.

No comments:

Post a Comment