Jumba watakaloishi wasanii wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba Bongo Star Search (BSS), likijulikana kama ‘BSS Kili House’ lilizinduliwa jijini Dsm mwishoni mwa wiki huku nyota 20 waliolamba zali la kutinga ndan
i ya mjengo huo wakianikwa hadharani.Akizungumzia ishu nzima ya mjengo huo...Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark, Rita Poulsen 'Madam Rita', alisema kupitia jumba hilo wasanii hao watapata mafunzo mbalimbali ya muziki na maisha kutoka kwa jopo la wataalamu wa fani hizo.
“Tunaamini mafunzo watakayoyapata ndani ya jumba hili, yatakuwa chachu ya wao kung’ara katika medani ya muziki na kuweza kujiajiri mara watakapokuwa wametoka kama ilivyo lengo la BSS, wakiwa chini uangalizi wa mama wa jumba hilo, msanii mkongwe wa fani ya uigizaji Natasha,” alisema Rita.
Alisema Benchmark imedhamiria kuibua vipaji vya wasanii ili waweze kujiajiri na kuepuka kujiingiza katika vitendo vya kihuni, jambo ambalo wamefanikiwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita tangu kuanzishwa kwa shindano hilo.
“Muziki ni ajira ambayo inaweza kubadilisha maisha ya vijana, iwapo watazingatia maadili ya fani hiyo na ndiyo maana tumekuwa tukiwekeza katika muziki, kwa kufanya shindano hili ambalo limeshawawezesha vijana mbalimbali kujiajiri,” alisema Rita.
Aidha, Rita alisema BSS ya mwaka huu imeboreshwa kwa kiwango cha kimataifa na itatoa mshindi ambaye anakidhi viwango vya kuwa mwanamuziki wa kimataifa.
Wasanii waliotinga 20 bora na kuingia katika kinyang’anyiro cha kusaka shilingi milioni 30 kwa mshindi wa shindano hilo ni Shafii Zubery, Juma Maliki, Christa Bela, Vasmo Onesmo, Chibi Dayo, Saidi Omary, Perus Doktan, Irene Haule, Abraham Magage, Saum Ramadhani na Salum Waziri.
Wengine ni Baby Johnson, James Martin, Haji Ramadhani, Ruth Oscar, Christabela Azoya, Winfrida Richard, Kakoye Hamson, Haji Ramadhani na Mariam Mohamedi.
No comments:
Post a Comment