October 05, 2010

Mwisho alikuwa ananitaka, Paloma adai:

.
Mshiriki wa Big Brother kutoka Zambia, Paloma amedai kuwa Mwisho kutoka Tanzania alijaribu kumtongoza lakini yeye alikuwa amemzimia kijana na Nigeria, Uti.Paloma alidai kuwa Mwisho ndiye aliyejaribu kumbusu
kabla ya kumvutia ndani ya Jacuzzi.

Meryl aliingilia kumtetea mchumba wake lakini Paloma aliendelea kudai kuwa Mwisho alikuwa akimtaka kimapenzi. Paloma alisema daima alikuwa akimuona Uti kuwa ni mwanaume mwenye mvuto lakini alibaini baadaye kwamba kijana huyo si aina ya wanaume anaowahitaji.

Sheila wa Kenya ndiye aliyeanzisha mjadala huo baada ya kumuuliza Paloma ni mwanaume gani aliyemzimia mjengoni na nani ambaye mwanadada huyo alimtongoza.
Paloma kisha akamuelezea Meryl kilichotokea kwenye Jacuzzi, na akakanusha kabisa kwamba alikuwa akijaribu kumtongoza Mwisho.

Vimwana hao walikuwa tayari wako kitandani baada ya sherehe yao ya wikiendi ambapo waliburudishwa kwa disko la DJ Waxxy. Paloma alisema hajawahi kuvutiwa na Mwisho lakini alikuwa ni shabiki wa kijana huyo wa Kitanzania tangu aliposhiriki katika Big Brother 1.

No comments:

Post a Comment