October 05, 2010

BSS 2010 kuzoa m30/-:

.
Mshindi wa Bongo Star Search, BSS, 2010, atazawadiwa shilingi milioni 30, mkurugenzi wa Benchmark Prudactions inayoandaa shindano hilo la kuimba, Rita Paulsen alisema juzi Ijumaa.Rita alitangaza zawadi hiyo katika
sherehe ya kuzindua nyumba maalumu yashindano hilo ya 'BSS Kill House' iliyopo Mikocheni Jijini Dar es salaam.

Washiriki wataishi kwa muda wa miezi miwili wakijifunza mambo mbalimbali ya kimaisha ikiwemo masuala ya muziki, alisema Rita.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Rita alisema Benchmark mwaka huu imeboresha zawadi ya mshindi huyo wa kwanza. Pascal Casian 'Baba Rita' alizoa shilingi milioni 25 katika shindano lililopita.
Aidha, washiriki walioingia 20 bora wataishi kwenye nyumba hiyo tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakikaa kwenye hoteli.

Alisema kuwa washiriki hao wakiwa kwenye nyumba hiyo ambayo imejengwa kwa udhamini wa bia ya Kilimanjaro watajifunza mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya muziki.

"Naweza kusema tangu tuanzishe shindano hili, mwaka huu ndiyo tumepiga hatua kubwa. Hivyo hawa washiriki 20 wataishi ndani ya nyumba hii huku wakijifunza mambo mbalimbali ya kimaisha," alisema Rita.
"Wakitoka humu watakuwa wamepata faida sana kwani hata mshindi atakayeshinda atakuwa amejua jinsi gani ya kutumia fedha zake."

Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa katika kipindi cha mkataba wao wa miaka mitatu wa kudhamini shindano hilo watahakikisha linaboreka na kuwa na ubora wa kiwango cha juu.
Rita alisema washindi 20 walio kambini walipatikana kutoka kwenye jumla ya washiriki 6,000 ambao walijitokeza kwenye mikoa mbalimbali.

Alisema kuwa washiriki hao walioingia kwenye 20 bora watakiwa wakionekana kupitia kwenye kituo cha televisheni cha ITV wakiwa wanaendelea na shughuli mbalimbali ndani ya nyumba hiyo.

No comments:

Post a Comment