September 22, 2010

Washindi watano wa Shindano la Chemsha Bongo kuzuru China.

Imeelezwa kuwa Serikali ya China na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika sekta ya habari ambapo shirika la habari la China (Xinhua News Agency) limekuwepo nchini kwa miaka mingi likiandika habari za maendeleo.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Utamaduni na Michezo Bwana Clement Mshana katika sherehe za kutuoa tuzo kwa washindi wa Chemsha Bongo kuhusu miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya
serikali ya China na Tanzania.
Bwana Mshana alisema licha ya kuwa na kukabiliana na propaganda za nchi za magharibi shirika la habari la China (Xinhua News Agency) limekuawa likiandika habari za maendeleo na kuongeza sauti ya nchi zinazoendelea.

Alisema vipindi vinavyotangazwa na shirika hilo kwa lugha ya Kiswahili vimesaidia kuimarisha ushirikiano na udugu uliopo kati ya Tanzania na Serikali ya China.

“Ni jambo la kufurahisha kuona kuwa kutokana na mawasiliano kati ya China na Tanzania katika sekta mbalimbali ,Watanzania wengi wamekuwa na hamu kubwa ya kuelewa mambo ya China hivyo kupelekea watu wengi kujifunza lugha ya Kichina.”.Alisema Mkurugenzi Mshana.
Alisema shindano la Tuzo kwa waandishi wa Chemsha Bongo lililoendeshwa kwa mara ya kwanza kwa mara ya kwanza kwa ushirikiano kati ya vyombo vya Habari vya China na Tanzania limeutangaza,limeelimisha na kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na China.
Katika hatua nyingine Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng mashindano ya Chemsha Bongo yalilenga kufuata moyo wa ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Afrika katika mambo ya Utamaduni

Alisema katika kuadhimisha miaka 45 ya uhusiano kati ya China na Tanzania Radio za China na Tanzania zimefanikiwa kufanya kufanya ushirikiano katika matangazo ya Chemsha Bongo hiyo zilitangaza vipindi mbalimbali vya utangazaji vya Kiswahili vya kukumbusha mchakato wa kukua kwa urafiki kati ya nchi ya China na Tanzania.

Balozi Xinsheng alifafanua kuwa Chemsha Bongo hiyo imeweka daraja la kuongeza urafiki,maelewano na mawasiliano kati ya wachina na watanzania na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa mikakati kati ya China na Tanzania.
Katika mashindano ya ya Chemsha Bongo Radio ya China ya kimataifa (CRI), TBC na Sauti ya Tanzania Zanzibar zilifanya ushirikiano katika kurusha matangazo ya shindano la Chemsha Bongo ambapo wasikilizaji walitakiwa kutoa mapendekezo kwa ajili ya kuendeleza zaidi kati ya China na Tanzania

Aidha mashindano hayo yalishirikisha zaidi ya wasikilizaji 1600 kutoka mikoa 20 ya Tanzania ambapo washindi watano maalum watakwenda kutembelea nchi ya China kwa siku kumi na washindi wa pili walipata zawadi ya Vereheni ambapo washindi wa tatu walipata zawadi ya Luninga za rangi.

No comments:

Post a Comment