September 22, 2010

Project Fame `ngoma` nzito!

Majaji wa mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba ya Tusker Project Fame, wamekuwa na wakati mgumu wa kuwapata washindi watano kwa upande wa Tanzania, baada ya washiriki 16 waliopita katika mchujo wa kwanza, kuonekana wana uwezo mkubwa wa uimbaji.
 
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ambayo inaendesha usaili huo nchini, Teddy Mapunda, alisema hadi jana majaji walikuwa hawajaweza kuwapata washindi wa shindano hilo lililofanyika kwenye Hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam watakaoenda Nairobi, Kenya kwa ajili kufanyiwa mchujo mwingine ili kuwapata wakali watatu watakaoingia kwenye fainali ya shindano hilo.

Alisema, kutokana na kuibuka kwa ugumu huo, majaji wameendelea kupitia upya mikanda ya video iliyorekodiwa wakati wa mchujo ili kuwapata washindi hao.

"Mwaka huu umekuwa tofauti na miaka ya nyuma, tumepata washindani na sio washiriki, hilo limetupa wakati mgumu sana hata kuwapata washiriki watano watakaoenda Nairobi," alisema.

Zoezi la kuwasaka washiriki hao lilifanyika kwa siku mbili kuanzia siku ya Jumamosi hadi Jumapili ya wiki iliyopita, ambapo jumla ya washirki 138 walijitokeza kufanyiwa usaili wa kuonyesha vipaji vyao vya uimbaji.

Source:

No comments:

Post a Comment