September 22, 2010

TMK na dongo kwa waliofulia!

Kundi la TMK Wanaume Family, limeachia wimbo wake mpya uitwao ‘Wapinzani’, unaoonekana kama kebehi kwa makundi yaliyofifia. Akiongea na DHW kwa njia ya simu jana, Meneja wa kundi hilo Said Fella, alisema kuwa, sababu ya kuutoa wimbo huo ni kutaka kuwahamasisha wasanii wa makundi mengine kuwa wavumilivu kama wao.
Fella alisema, katika wimbo huo ulioimbwa na wasanii wote wa kundi hilo, pia wameamua kumshirikishamsanii Shaban Katwila ‘Q. Chilla, kwa nia ya kuonyesha mshikamano wao na wasanii binafsi au makundimengine.

“Mkubwa tumeachia wimbo mpya unaitwa ‘Wapinzani’ tumeshausambaza kwenye vituo vya radio, hatujamtukana mtu, ila tunachokifanya ni kuwapa wenzetu ushauri wa kufanya kazi kwa bidii na bila kuchokakwa faida ya muziki wetu,” alisema Fella.

Alisema, wimbo huo utakuwa katika albamu ijayo ya kundi hilo, ambayo wameanza kuiandaa wakitarajiakuitoa baadaye mwaka huu.
Source: Darhotwire.com

No comments:

Post a Comment