September 25, 2010

Mwisho Na Meryl Kuvishana Pete Za Uchumba Leo

Mshiriki wa Jumba la Big Brother kutoka Tanzania, Mwisho Mwampamba na kimwana wake kutoka Namibia, Meryl, wanatarajia kuvishana pete ya uchumba leo, katika tukio linaloaminika kuwa litaweka historia mpya katika mashindano hayo ya runinga.

Mwisho ameikaribisha siku yake kubwa maishani kwa kushinda mashindano ya kuwania kuwa kiongozi wa jumba kwa wiki hii.

Mtanzania huyo, na Meryl walimstua Big Brother wakati walipomweleza wiki kwamba wanatarajia kufunga ndoa ndani ya jumba hilo.

Hata hivyo, baada ya majadiliano ya mara kwa mara baina yao ikiwa ni pamoja na kuzungumza na Biggie, wawili hao walikubaliana kwamba ni vyema wakavalishana pete za uchumba tu na kwamba ndoa ni jambo linalohitaji ndugu wa familia za pande zote mbili ambao hawaezi kupatikana ndani ya jumba hilo.

Mwisho alikuwa amejilaza kitandani na Meryl wakati Big Brother alipotangaza mshindi wa shindano la kupata kiongozi wa nyuma wa wiki hii ijayo.

Kijana huyo Mtanzania alipata busu la pongezi kutoka kwa Meryl na akasema inategemea kama ataepuka kutolewa mjengoni wiki hii.

Afrika inasubiri kuona tukio la kwanza na la aina yake ndani ya jumba hilo la Mwisho kumvisha pete ya uchumba Meryl. Biggie amewaahidi washiriki hao kuwasaidia katika kufanikisha sherehe yao ya uchumba leo.

No comments:

Post a Comment