December 07, 2011

Willow Smith Atangaza Tarehe Ya Kutoka Kwa Albam Yake.


2012 itakuwa ni mwaka mpya kwa Willow Smith. Mtoto mwenye miaka 11 na mwenye kipaji cha kutisha katika game ya muziki, hatimaye ametangaza ujio wa albam yake mpya itakayoingia sokoni mapema mwakani.


Akiwa katika interview ndani ya kipindi cha burudani kwa vijana “106 & Park,” kinachorushwa na BET Willow ametangaza kwamba atakua akiingiza sokoni albam yake ya kwanza April 3, 2012. Albam hii iliyocheleweshwa mara kadhaa, kutokana na kuhamia lebel ya Roc Nation, ameshaachia ngoma kali kama “Whip My Hair,” “21st Century Girl,” na mzigo mpya uitwao “Fireball” alioshirikiana na Nicki Minaj.

Video ya mahojiano yake na “106 & Park.” itaoneshwa kwa mara ya kwanza wiki hii. Na hapa ni maelezo ya Willlow kuhusu kuja na albam yake kama msanii mpya.

No comments:

Post a Comment