December 06, 2011

Rihanna, Mary J. Blige Waingia Katika Top 5 Ya Albums Chart Ndani Ya Billboard.

Rihanna na Mary J. Blige wamefanikiwa kuzitikisa chart za albam bora wiki hii. Warembo hawa wako katika wakati mzuri wa kutabasamu kwasasa baada ya albam zao kufanya vizuri katika mauzo, na kuwaweka katika orodha ya top 5.


Albam ya sita kutoka kwa The Barbados pop star’s Rihanna iitwayo Talk That Talk ikiwa imeshika nafasi   No. 3 ndani ya Billboard Top 200 kwa kuuza nakala ya 197,000 katika wiki ya kwanza, na hii ni kwa mujibu wa "Nielsen SoundScan

Albam yake hii inamfanya Rihanna kuingiza jumla ya albam zake zote katika Top 10 na  huku ikiwa nyuma ya albam ya LOUD iliyouza nakala 207,000 mwezi November mwaka jana.

Na miaka 17 baada ya kutoka na albam yake ya breakthrough My Life, Mary J. Blige amethibitisha tena kwamba yeye ni mkali na ana uwezo wa kushindana na kizazi kipya. My Life II… The Journey Continues (Act I), ni uthibitisho wa albam kali ya Queen of Hip-Hop Soul’s tangu mwaka 1994, ikiwa katika No. 5 kwa kuuza 156,000.

Wakati huo huo Drake  akiwa na albam yake ya pili "Take Care" iko katika nafasi ya nne kuelekea nafasi ya 1, kwa kuuza nakala 173,000 katika wiki yake pili ikiwa chini ya malengo kwa 73%.

No comments:

Post a Comment