December 07, 2011

LL Cool J Aizungumzia Single Yake Na Ne-Yo

Rapa ambae ni halali kumuita legend wa hiphop duniani LL COOL j, amesema hakua na mpango wa kuitoa kwenye radio na mitandao mingine track yake ya NO MORE aliyompa shavu mwimbaji NE Y0, ila alifanya hivyo kutokana na watu kuipenda hiyo track baada ya kuisikia kwenye TV SERIES ya NCIS Las angeles.


Ll cool J mwenye umri wa miaka 43, ambae sasa hivi amejiweka sana kwenye kucheza movie na TV series na kuuacha muziki mbali kidogo, hajasikika kwenye single yoyote redion kwa kama miaka mi3 au minne mpaka sasa.

Mpaka sasa LL cool j amecheza kwenye TV SERIES 10, na amecheza movie 23 toka aanze kuigiza miaka 26 iliyopita.

Asilimia kubwa ya Utajiri alionao umetokana na kuigiza movie, na inasemekana ndio sababu kuu inayomfanya afanye movie zaidi kuliko muziki, kwa sababu movie inalipa zaidi.

No comments:

Post a Comment