December 04, 2011

CPU: movie ya kibongo inayoshine CINEMA!!

Movie ilyotengenezwa kwa Gharama bajeti kubwa bongo, ikiaminika kwamba ndio movie ya kibongo kuandaliwa kwa muda mrefu kuliko movie nyingine yoyote imeonyesha mafanikio toka ianzwe kuonyeshwa kwenye ukumbi wa CINEMA Dar es salaam.

Ismail Katumda mmoja wa waandaaji wa MOVIE hiyo amesema toka movie hiyo imeanzwa kuonyeshwa CINEMA tarehe 25 mwezi uliopita, mpaka juzi, kila siku ticket zimekua zikinunuliwa zote na haibaki hata moja, na hata leo kwenye mida ya saa12 alipozungumza na FIXED 20 ticket za watu kuingia kuichek hiyo movie zilikua zimeuzwa nusu.

CPU ni movie iliyochezwa kwenye jiji la DAR ES SALAAM peke yake, na imepigwa kwenye zaidi ya location 32, huku picha zake nyingi zikipigwa kutoka angani kupitia HELCOPTER.

stori yake inahusiana na watoto wa mtaani, haina action wala mapenzi lakini inasemekana ni movie inayovutia sana kwa jinsi ilivyochezwa kihisia.

hii inakua movie ya pili ya kibongo kuonyeshwa kwenye ukumbi wa CINEMA Tanzania.

No comments:

Post a Comment