December 07, 2011

Lil Wayne Amezifuta Ziara Zake Nchini Australia Na Kuongeza Tarehe Za Ziara Barani Afrika;

Rapper Lil Wayne amewashtua mashabiki wake wa Australia baada ya kufuta tarehe za ziara za kimuziki nchini. Rapa huyo alitakiwa kufanya show huko Perth (November 25) lakini akaifuta show, pia alikuwa na show huko Adelaide jumapili ya (November 27) lakini pia akaifuta.


Msemaji wa Lil Wayne’s akaongeza kwamba (November 29) alitakiwa kufanya show huko Melbourne,  lakini ilibidi aifute show hiyo kutokana na kuingiliana kwa ratiba zake.

Kwa mujibu wa taarifa, Lil Wayne alikuwa na show na Eminem katika uwanja wa Etihad Stadium siku ya juzi yaani December 1.

baadaye mwezi huu, Lil Wayne atakuwa na zaira ya muziki barani  Africa kwa muda mrefu sana, na hii itakuwa ni ziara ya kwanza kwake kufanya show huko Motherland.

Na December 7, Lil Wayne atakuwa jiji la Cape Town, South Africa, kwaajili ya show huko Bellville Velodrome.

Na baada ya hapo atakwenda Johannesburg siku ya Ijumaa ya December 9 na kufanya bonge moja la show ndani ya Coca-Cola Dome, na itafuatiwa na show nyingine iliyoongezwa huko Durban December 11 ndani ya ukumbi wa Wavehouse.

Na taarifa zaidi kutoka YMCMB  zinaeleza kwamba show zote Africa zitawahusisha member wa kundi la Young Money kama Mack Maine, Gudda Gudda, Corey Gunz, Shanelle, Jae Millz na T-Streets.

Tickets kwaajili ya show za Africa tayari zinauzwa kupitia mtandao wa Computicket.

No comments:

Post a Comment