December 06, 2011

Hili Choko Choko

BADO chokochoko kati ya masistaduu wawili ‘wanaotikisa mkia’ katika Tasnia ya Filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ zinaendelea huku kisa kikidaiwa kuwa ni mapenzi, Fixed 20 inakuja na full data.


Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na wawili hao, tangu walipopeana za uso laivu wakitaka kupigana chupa miezi kadhaa iliyopita walipokutana kwenye ‘pub’ ya mwigizaji mwenzao, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ maeneo ya Komakoma Mwananyamala, Dar es Salaam, waligeuka chui na paka hadi leo. 

Chanzo hicho kilikumbushia kuwa sababu kubwa ni wivu wa kimapenzi ambapo ilidaiwa kwamba Wolper alikuwa na mpenzi wake ambaye alikorofishana naye na Kabula kutumia ‘chansi’ hiyo kujichukulia kiulaini kama ananawa.

Chanzo hicho kisicho na simile kilimtonya paparazi wetu kuwa, baada ya bifu lao kuripotiwa kwenye magazeti pendwa, Wolper aliendelea ‘kuchati’ kwa meseji na mpenzi wake huyo ambapo Kabula alizinasa, ndipo akagundua Wolper alitaka ‘kurejesha majeshi’ hivyo akaamua kukomaa na sasa ndiye mmiliki wa mpenzi huyo.

Ilidaiwa kuwa, ili kujihakikishia umiliki wa mpenzi huyo, Kabula aliunda ‘Al-Shabaab’ yake yenye wasichana ‘micharuko’, lengo likiwa ni kumshughulikia Wolper popote watakapomtia mikononi, lakini hakufanikiwa.

Baada ya kunyaka mchapo huo, mwandishi wetu alimtafuta Kabula na kumsomea ‘eituzedi’ ya unyambilisi anaouendesha juu ya Wolper ambapo alifunguka: “Sihitaji kusikia wala kuzungumza chochote kuhusu Wolper kwa sababu siwezi kuelewana naye hadi kiyama, labda umuulize yeye kwa nini hatupatani.” 

Alipoulizwa juu ya kuunda kundi la kumchapa Wolper huku akijua ni kujichukulia sheria mkononi, Kabula alitamba: “Niunde kundi la nini? Mimi mwenyewe ni jeshi tosha kwani akiniletea za kuleta tukikutana namharibia vibaya.”

Ili kupata mzani wa taarifa hiyo, FIXED 20 ilimtafuta Wolper na kumpa mchongo kamili ambapo alijibu kwa mkato: “He! Jamani mimi siongei na Kabula.”

No comments:

Post a Comment