December 06, 2011

Wema Asema Hataki Kwenda Tena South Afrika

DIVA katika Tasnia ya Filamu Bongo, Wema Abraham Sepetu amesema hali aliyoiona nchini Afrika Kusini inatisha na hana hamu ya kurudi tena nchini humo.


Wema amesema hayo hivi karibuni, ikiwa ni siku chache baada ya kurejea nchini akitokea Afrika Kusini alipokwenda na mpenzi wake, kinda anayefunika katika Bongo Fleva Naseeb Abdul ‘Diamond’ kwa mapumziko mafupi, akisisitiza kwamba matukio aliyoyaona yamempa hofu kubwa. 

“Kwa kweli kunatisha, nimeshuhudia mtu akipigwa risasi mbele ya macho yangu. Cha kushangaza, hakuna mtu aliyejishughulisha na tukio hilo ambalo lilitokea mtaani kabisa, tena mchana,” alisema na kuongeza: “Hapa Bongo tuna amani, kule inavyoonekana kama umegombana na mtu, anatoa bastola na kukufyatulia risasi na hakuna atakayeamulia. Kwa kweli nimekuwa na hofu sana na sitamani kwenda tena.”

No comments:

Post a Comment