December 07, 2011

Professor Jay Kujenga Studio Nyumbani Kwake!!

Siku chache baada ya kuhamia kwenye nyumba yake aliyojenga mbezi ya kimara dare s salaam, Hiphop Legend wa TANZANIA Profesa J, ameFIX kwamba mpango unaofata ni kujenga studio ya muziki nyumbani kwake.


Kutokana Na Kufatwa Sana Nyumbani Kwake Na Wasanii Wachanga Wanaohitaji Msaada Wake, Prof Amesema Lengo Ni Kufaham Vipaji Vipya Na Kuwawezesha Kupitia Profesa Jay Foundation For Tanzania Community.

kuhusu kuproduce nyimbo yeye mwenyewe, Prof amesema hayuko vizuri kwenye swala la upigaji wa vyombo ila ataweka mawazo yake mengi katika record yoyote, atakachokifanya baada ya kujenga studio ni kutafuta producer mzuri kwa ajili ya kudil na hiyo kazi.

bado haijajulikana ataianzisha lini rasmi hiyo wala itakamilika lini kwa sababu hata ujenzi bado haujaanza ila mpango uko mbioni.

No comments:

Post a Comment