December 06, 2011

Facebook Yazidi Kumtesa Linnah!

Stori ambayo ilimfanya aingie kwenye habari za leo kwenye FIXED 20, ni kuhusu account mpya zilizofunguliwa na watu wasiojulikana, kwa kutumia jina lake kwenye fb.


Linah amesema “sijui nina kosa gani kwa baadhi ya watu ambao wameonekana kunichukia bure wakati hata sina hatia, kuna watu wamefungua account mbili za facebook kwa kutumia jina langu, LINAH SANGA na wanatukana watu na kuwajibu vibaya, kuna mambo mengi sana ya ajabu wanayafanya mpaka yanapelekea mimi nagombana na BOSS wangu”

Linah amesema sasa hivi hata huwezi kizitofautisha hizo account feki na account yake halali, manake hao jamaa wanamfatilia sana Linah hata akibadilisha picha ya profile na wao wanabadilisha na kuweka aliyoweka Linah.

No comments:

Post a Comment