December 07, 2011

Sasa Hapa Tusemaje! Wanawake Wa Zimbabwe Wanabaka Wanaume!!!!

Polisi Wa Zimbabwe Wanaamini Kwamba Kuna Tabia Ya Wanawake Kubaka Wanaume Nchini Humo Na Kutumia Mbegu Zao Za Kiume Kwenye Imani Za Kishirikina Kwa Ajili Ya Utajiri.


Imechukua zaidi ya mwaka mmoja polisi kuwakamata wahusika ambao juzi, baadhi yao wamefikishwa mahakamani Harare kwa mashtaka ambayo yameishangaza nchi nzima.

Mtu mmoja aliyewahi kubakwa na wanawake hao, amesema ilitokea wakati alipopewa lifti na kundi la wanawake watatu kwenye mji wa Harare ambapo Mmoja wa wanawake hao alimrushia maji usoni na baadae wakampiga sindano iliyompa hamu ya kufanya ngono.

Waliisimamisha gari na kumlazimisha kufanya ngono na kila mmoja wao kwa kutumia kondom, Baada ya kumaliza shughuli yao walimuacha msituni akiwa uchi.

1 comment:

  1. Harrah's Casino Hotel Atlantic City, NJ - Mapyro
    The 안동 출장안마 Harrah's Atlantic 제천 출장마사지 City Hotel & 밀양 출장마사지 Casino is a casino hotel 논산 출장안마 located in the marina district of Atlantic 문경 출장샵 City, New Jersey.

    ReplyDelete