December 07, 2011

50 Cent Kutoka Na Mixtape Ya Ngoma 10 Ambayo Itaitwa 'Big 10'

The Hip-Hop Mogul mwenye asili ya Southside Jamaica, mzaliwa wa jimbo la Queens rapper 50 Cent yuko mbioni kuachia mixtape yake aliyoipa jina la “Big 10.”


Kwa mujibu wa 50, mixtape hii inakuwa ni kwasababu ya kusherekea miaka 10 tangu atoe mixtape yake ya  “50 Cent is the Future” iliyotoka mwaka 2002 na kutikisa vituo vya internet kwa mauzo kwa waketi ule.

“Ni miaka 10 sasa tangu nilipotao mixtape ya 50 Cent is the Future,” 50 Cent aliandika kupitia twitter. “Hivyo nakuja na ‘BIG 10′ wiki ijayo tarck 10 kali #SK.”

Rapa huyo kutoka New York ambaye amekuwa kimya sana kwenye game, pia alitangaza kwamba yuko katika maandalizi ya kutoka na kitabu cha “Playground” wakati akiwa kwenye mahojiano na “Piers Morgan.”

50 pia yuko kwenye plan za kuachia albam yake ya Black Magic, huku akifanya mpango wa kufanya video kibao, ambazo zitakua ni kwa kila wimbo atakao utoa.

“Ninafanya shooting kwa kila wimbo nitakao utoa. The BIG 10 mixtape ni kwaajili ya wenye chuki juu yangu #SK,” 50 Cent aliandika tena kupitia twitter.

50 kwasasa yuko busy na kuikamilisha albam yake ya 5 na juzi kati Dec 3 alikuwa akiifanyia promo drama yake ya “All Things Fall Apart,” kupitia BET.

No comments:

Post a Comment