December 06, 2011

Peter Msechu Awafungukia Mapromoter Wa Tanzania

MSHINDI wa Project Fame 2011,  Peter Msechu ameibuka na kusema: “Mapromota wa Bongo wamenisahau kabisa, pamoja na ukali wangu, lakini hawanialiki kupiga shoo. Nimejiuliza sana sababu, lakini sijapata jibu.” Msechu alisema hayo juzikati jijini Dar es Salaam, ambapo alisisitiza: “Wakati Bongo wakinibania, naitwa sana nje ya nchi. 


Kwa mfano Kenya, nafanya shoo nyingi sana lakini hapa nyumbani hawanipi dili.” Mwanamuziki huyo ambaye ni zao la Shindano la Bongo Star Search anayetesa na kibao cha Relax akiwa amepiga kolabo na msanii Kidumu kutoka Kenya, amewataka mapromota wa Bongo kuacha ubaguzi badala yake wazingatie ubora wa kazi.

No comments:

Post a Comment