June 06, 2011

POLE SANA....INSPECTOR HAROUN...!

Haruna Kahuna aka Inspector aka Babu za chini ya maji zinadai kuwa mke wake Bahati Shada ameyetoweka home pande za Tandika,
Dar es Salaam kwenye mazingira ya kutatanisha akiaga anakwenda kuteka maji bombani Inspector alifunguka kuwa yeye alikuwa kwenye kikao cha kuzindua upya kundi lao la Gangwe Mob na aliporudi nyumbani majirani walimtonya kuwa,wife wake akitoka na ndoo ya maji wakadhani anakwenda bombani na mpaka saa 3 usiku alikua hajarudisha timu nyumbani,Na Inspector akionesha kuingiwa na hofu na alitoa taarifa polisi na Serikali ya mtaa,ila alifunguka kuwa siku moja kabla ya kutoweka walikwaruzana kidogo juu ya utaratibu wake wa kuchelewesha chakula cha usiku,na anahofia kuwepo kwa mazingira ya uchawi na alikua na mpango wa kwenda kumtafuta mke wake pande za Uzaramuni
….POLE SANA BABU....TUNAKUOMBEA NDOA ISIWE NA DOA...!

No comments:

Post a Comment