May 31, 2011

K-BAZIL KUZINDUA ALBUM YAKE YA GOSPEL...!


KASHUMBA BAZIL AKA K-BAZIL
Msanii wa Bongo Flava aliyetamba sana na track iliyojulikana kwa jina la Riziki,featuring Stara Thomas na Bizman ,Kashumba Basil aka K-Bazil anatarajiwa kuzindua album yake ya kwanza ya Gospel aka Injili

K-Bazil alitangaza kuokoka mwaka 2008 na mwaka 2010 akawa mchungaji na yuko mbioni kutoa album yake ya kwanza ya muziki wa Injili

Album ya Injili ya K-Bazil inaitwa Yesu Ananipenda,yenye track 10 Tamasha lake la kwanza la Uzinduzi litafanyika mkoani Iringa,siku ya Jumapili ya tarehe 5 Juni,2011 na baada ya hapo atazunguka mikoa mingine kama Mbeya, Morogoro,Dodoma, Arusha,Kilimanjaro na mikoa mingine na litakuja kumalizika katika mkoa wa Dar es salaam mwezi wa July na nia ni kuchangisha michango ili kusaidia watu wasiojiweza na walio katika mazingira magumu kama watoto yatima,wazee,wajane,walemavu nk.Na K-Bazil amefunguka kuwa hiyo ndio njia yake ya pekee ya yeye kumshukuru Mungu kwa neema ya wokovu aliyompatia na kupita kwenye mikoa aliyowahi kupita akiwa anafanya Bomgo Flava nia ni kuifuta ile historia yake ya muziki wa Bongo fleva na kuwatambulisha watu kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu sasa na amesimama kweli katika Imani yake na anampenda Yesu pia!

No comments:

Post a Comment