May 31, 2011

Pacha Wa P Square Aporwa Na Majambazi!!!


PAUL OKOYE - P SQUARE
Mmoja wa pacha wanaounda kundi la P-Square,Paul Okoye alionja joto ya jiwe baada ya kuvamiwa na majambazi alipokuwa njiani kuelekea Victoria Island kucheki washikaji zake Paul alikuwa
 akiendesha mkoko wake mpya aina ya BMW X6 lenye plate number za "RUDE BOY"na kwa moyo wa utu aliokua nao ndio uliomponza,coz alisimama njiani kutoa msaada kwa waliopata ajali na watu wawili kutokea pasipojulikana na kumtolea bastola na kumpora simu,fedha na vito vya thamani na vinginevyo

....GARI YA PAUL OKOYE....BMW X6-RUDE BOY....
Paul alifunguka kuwa baada ya watu hao kuchukua walichotaka,walitaka pia kuchukua funguo ya gari ndipo alipopata msaada wa mama mmoja kupiga kelele na kusababisha waporaji hao kusepa na kushindwa kupora gari lake.

No comments:

Post a Comment