June 06, 2011

RIRI AIBUKA.....AITETEA VIDEO YA MAN DOWN...!

ROBYN RIHANNA FENTY AKA RIRI
Baada ya fans wa Rihanna kutaka video yake mpya ya Man Down ifungiwe coz itahamasisha uhalifu kwa madogo,baada ya Rihanna kuonekana
mwanzo wa video hiyo akimpiga risasi mshikaji mmoja hivi,huyo jamaa wa kwenye video ameibuka na kufunguka kuwa yeye alianza kumshambulia RiRi na alipopigwa risasi ilikua ni kulipiza kisasi baada ya kumbaka Rihanna 'behind the scenes' wala watu wasielewe vingine!
Rihanna mwenye alifunguka kwenye Tweeter alijitetea kuwa “yeye ni rockstar mwenye miaka 23 na hana watoto,inakuaje watu wanamchukulia yeye kama mzazi? Na hatuwezi kuwafundisha watoto kitu gani cha kufuata kwa dunia ya sasa”
....JAMAA BAADA YA KUPIGWA RISASI...KWENYE VIDEO YA MAN DOWN..!
Video ya Man Dow,ilitengenezwa Jamaica na ilioneshwa kwa mara ya kwanza na BET Television na kupata upinzani mkubwa sana toka kwa The Parents Television Council kwa kuitaka video hiyo ifungiwe coz itasababisha vijana wengine wadogo kuingia kwenye uvunjifu wa amani

No comments:

Post a Comment