June 08, 2011

BAJETI YA 2011/12 KUSOMWA LEO JIONI....MJENGONI...!


Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza jana mjini Dodoma ikiwa ni Bunge la Bajeti wa mwaka 2011/12,kwa kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu na shughuli nyingine za bunge na Bajeti
wa mwaka 2011/12 inatarajiwa kusomwa leo saa 10 na Waziri wa Fedha na Uchumi,Mh Mustapha Mkulo....
MUSTAPHA MKULO - WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI
Kambi ya upinzani pia itawasilisha bajeti yake bungeni ambapo bajeti hiyo imeipa kipaumbele kufutwa kwa posho za vikao vya serikali na za bungeni ili kuipunguzia serikali mzigo bajeti itakayowasilishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Kabwe Zitto
ZITTO KABWE - MBUNGE KIGOMA KASKAZINI/WAZIRI KIVULI - FEDHA NA UCHUMI
Bajeti hiyo inatarajiwa kusikilizwa masikioni na watanzania waliowengi huku Watanzania wakiomba kuangalia zaidi maisha ya kila siku ya mtanzania kwa kupunguza bei za vyakula ,mafuta ili kuleta unafuu kwa maisha na watanzania wengi wakionekana kulalamikia ugumu wa maisha unaopanda kila kukicha

No comments:

Post a Comment