Anayeaminika kuwa mganga wa Freestyle hapa Bongo...namzungumzia Ngwair..amekiri kuwa game imekaza (ngumu) ile kinoma kwenye muziki...na kudai kuwa mashabiki wamekuwa wajanja mno.
Ngwair anaendelea kuweka wazi kuwa muziki wa sasa hauangalii jina kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo baadhi walikuwa wakitoa nyimbo za ajabu ajabu na kuendelea kubaki kwenye chati.
"Muziki wa sasa umekuwa mgumu sana, si kama kipindi cha nyuma, hivi sasa watu wanaangalia kazi nzuri na wanajua ndio maana utaona sapoti wanayotupa hata tukipanda jukwaani ni kubwa," anasema, Ngwea ambaye jina lake halisi ni Albert Mangwea
"Kama hufanyi kitu cha maana utashangaa unapanda jukwaani wanakuangalia tu, lakini kama unafanya mambo ya uhakika watakupenda sana na hata mauzo yatakuwa mazuri. Jina au umaarufu havisaidii, cha muhimu ni kazi tu.
"Nimetulia kidogo, nataka niachie nyimbo zilizoko kwenye albamu yangu iliyopo sokoni kwa vile nyingi hazifahamiki lakini ni nzuri, ninazo mpya pia ambazo zitakuwa kwenye albamu ambayo naweza kuitoa Desemba.
"Siangalii fedha, soko la muziki ni gumu na kila mtu anajua hilo ndio maana nimeamua nitakuwa natoa albamu kwa ajili ya mashabiki wangu kwavile wananijali na wananipa sapoti.
"Fedha nitapata tu hata kwa njia nyingine, siwezi kutegemea muziki kuishi. Wala kimya changu hakimaanishi nimeishiwa kazi au chochote kile nafanya mambo kwa mpangilio, watu wangu wasiwe na wasiwasi mambo yanaenda vizuri."

No comments:
Post a Comment