September 29, 2010

Poteza Studio kuinua vipaji Temeke:

WASANII wenye vipaji katika medani ya muziki wa kizazi kipya kutoka maeneo mbalimbali ya Temeke, wanatarajiwa kuibuliwa katika mpango maalumu utakaoendeshwa na Studio za Poteza. Akizungumza na blog hii kutoka jijini Dar es Salaam juzi, Meneja wa studio hizo, Yusuf

Chambuso, alisema kuwa nia yao ni kuhakikisha wanawasaidia vijana wote wenye vipaji kutoka. Alisema kuwa ili kuwapata wasanii wenye vipaji na wasio na uwezo, wataandaa onyesho maalumu ambalo chipukizi hao wataonyesha vipaji vyao na watakaofanya vizuri wataendelezwa.

Alisema, kwa sasa wameanza mazungumzo na wamiliki wa kumbi mbalimbali na huenda wakautumia ukumbi wa CCM Kata ya 14 Temeke kwa mchujo huo.

“Mkubwa tumepanga kuanza kuwasaidia vijana wenye vipaji lakini ambao bado hawajatoka, tutawarekodia nyimbo  zao bure,” alisema Chambuso.

Alisema wameamua kufanya hivyo wakiamini kuwa, mafanikio ya wasanii hao hapo baadaye yatakuwa ni mafanikio ya Temeke kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment