September 29, 2010

Vodacom Miss Tanzania 2010 akabidhiwa bendera:

Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel akiwa ameshikilia bendera mara baada ya kukabidhia rasmi leo tayari kwa safari yake ya kuelekea nchini China katika jiji la Sanya ambako shindano la dunia Miss World 2010 linatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini humo Vodacom Miss Tanzania ataondoka kesho kwa ndege ya Shirika la ndege la Quatar Airways akipitia Uarabuni, Mongolia na kisha Sanya nchini China.
Esther Mkwizu ambaye ni Mwenyekiti wa Sekta Binafsi na aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi bendera ya taifa kwa Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel akikabidhi bendera hiyo huku wazazi wa Genevive wakishuhudia kulia ni baba yake Bw. Emmanuel Mpangala na kushoto ni mama yake mary.
Mgeni rasmi Esther Mkwizu ambaye ni Mwenyekiti wa Sekta Binafsi wa pili kutoka kushoto akimkabidhi bendera ya taifa Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera iliyofanyika kwenye ofisi za Kituo cha Uwekezaji TIC jijini Dar es salaam kushoto ni Mkurugenzi wa TIC Dr.Emmanuel Ole Naiko, kuliani Mkurugenzi wa Utamaduni na Kaimu katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Prof Helmas Mwansoko na katikati ni Mkuu wa Udhamini Vodacom Tanzania George Rwehumbiza.
Wadau Ibrahim Kaude Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania na Mtaalam wa habari Vodacom Tanzania Matina Nkurlu kulia walikuwepo katika hafla ya kumkabidhi bendera ya Taifa Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel katika ofisi za kituo cha uwekezaji TIC leo.
 
Source: Fullshangwe Blog

No comments:

Post a Comment