September 29, 2010

Witnes aomba kura za Watanzania:

MSANII wa Kizazi kipya hapa nchini, Witness Mwaijagwa ‘Witnes’ amewaomba Watanzania kumpigia kura, ili aweze kuibuka na ushindi wa tuzo za Chanel O za wimbo bora wa hip hop,
zitakazofanyika Novemba mwaka huu, Afrika Kusini.

Witnes ni miongoni mwa wasanii wa Afrika waliochaguliwa kuwania tuzo hizo kupitia wimbo wake wa Antention Please, akiwemo msanii mwingine Sara ‘Shaa’. Akizungumza na K.D.O.S Kutoka Dar es Salaam jana, msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao hicho, alisema kama atapigiwa kura na Watanzania wengi, ana uhakika wa kushinda tuzo hizo kutokana na ubora wa wimbo wake.

Alisema mpiga kura anaombwa kuchangia kura yake kwa kuandika neno 1B, kwenda namba +27839208406 na kwa uhakika zaidi andika www.witnes.com kujua kama kura yako imefanikiwa.

Alisema kwa njia ya mtandao mpiga kura anatuma neno hilo kwenda www.ChanelO.Tz kura yake itakuwa imefanikiwa kumpatia ushindi katika tuzo hizo kubwa barani Afrika. Hata hivyo msanii huyo, aliwataka Watanzania kukaa mkao wa kula kuangalia video yake mpya ya wimbo wake wa Player, ambao anauandaa hivi sasa na utakuwa tayari hewani kabla hajatimkia Afrika Kusini kuwania tuzo hizo.

Mbali na Witness, wasanii wengine wa Afrika waliotajwa kushiriki katika tuzo hizo ni D Banj, Wyre, Dj Cleo, K’naan wa Somalia, Namless, Bantwin na wengine wengi.

Source: Majira

No comments:

Post a Comment