October 01, 2010

BET AWARDS 2010 NA OKOA MABINTI KAMPENI: MZIGO KUPIGWA JUMAPILI HII U.S.OF OBAMA!!!


Mwanadada chuma kikali katika R&B/Soul crooner Chrisette Michele amekula shavu la kwanza la kuwa msemaji katika Zoezi la uzinduzi la kitabu kipya cha  “Saving Our Daughters”ikiwa ni kampeni itakayoendeshwa katika kusaidia jamii kupitia mauzo ya kitabu hicho


Eneo la tukio litakuwa ni kampas ya Clark Aon katika chuo kikuu cha Los Angeles ambapo mwanadada huyo atasimamia show hio ya Hip-Hop 4 Education Initiative Itayoenda pamoja na Wiki ya utoaji tuzo za BET siku ya jumapili Oct 3 mwaka huu

Info ni kwamba kwa washkaji wa Kitaa cha Los Angeles ambao watakuwa hawana Faranga za kutosha show itakuwa upande wao kwani itakuwa hakuna kiingilio huku wakipata nafasi ya kujumuika na Maselebrities wa kutosha ambao pia wameshapokea barua za mualiko

Katika kuhamasisha zaidi vijana wa kishule na wapenda Hip hop ni kwamba watoto wote wakishule watakahudhuria uzinduzi huo watapewa nafasi ya kuchagua ya kusoma moja kati ya vipande katika kitabu hicho

Kinachofanyika kwa sasa ni kwamba mwanadada huyo amesema ameamua kutoa saport kwa washkaji walioandika kitabu hichoo pamoja na kuanzisha mnpangoi wa Follow The Leader ambao unatajwa kuwa na Lengo lakuamsha hamasa miongoni mwa jamii

Kwa sasa Chrisette Michele anajiandaa kuachia Albamu yake mpya Nov 30 mwaka huu ambayo tayari matayrisho yake yameashaanza baada ya kuachia Single ya kwanza iitwayo I’m a Star,ilioandikwa na Ne-Yo

Hebu tukumbuke Kampeni zilizowahi kufanywa na Wasanii wa Bongo kuhusu haya mambo,Unaikumbuka Hip Hop Bila Madawa,Unaikumbuka Okoa Hip Hop, Back 2 The Hip Hop Summit

No comments:

Post a Comment