September 27, 2010

Uchumba wa Mwisho, Meryl wazua chuki zizini:

Mwisho na Meryl hatimaye ni wachumba rasmi. Huku akitetemeka, Mwisho alipiga goti na kumuuliza Meryl kama atakubali wafunge ndoa na bila ya kujiuliza kimwana huyo wa Namibia alijibu "Nitapenda baby" na Mwisho
alitoa pete yake ya madini ya Tanzanite na kumvisha kidoleni.

Katika hotuba yake, Mwisho aliweka wazi kwamba yeye hatokei kwenye familia ya kimahaba sana. “Kosa lolote nitakalofanya hapa, naamini nina muda mrefu maishani wa kufanya mambo mazuri,” Mwisho aliwahakikishia wakati walioshuhudia sherehe hiyo huku akicheka.
Wawili hao kisha wakabusiana midomoni.

Shangazi wa Meryl, Jamela, alionekana amejaa shaka kama jambo hilo lilikuwa ni 'siriasi' ama masihara na Meryl akamhakikishia kwamba jambo hilo ni 'siriasi' kabisa na kwamba hakuna wa kuwahukumu ila ni mapenzi yao na Mungu.
Meryl alisema anafahamu kwamba watu wana maoni tofauti kuhusu uchumba wao.
“Watu pekee wa kujibu katika hili ni sisi wewe. Tumeamua kwamba tunatumia maisha yetu yote yaliyobaki pamoja,” Meryl alisema.

Meryl aliongeza kuwa Mungu alipanga kwamba watakutana katika Big Brother All Stars kwa sababu wote walishaonana na kupendana katika televisheni. Shangazi wa Meryl, alimsaidia wakati akizungumza kwa kusema “yalikuwa ni mapenzi kwa baada ya kuonana mara moja.”

CHUKI ZIZINI

Wakazi wa zizini walionekana kujawa na chuki kutokana na tukio la Mwisho na Meryl kufunga uchumba.

Washiriki hao waliotolewa mjengoni siku za nyuma na kutupwa kwenye Zizi, ambako wanaishi na wanyama walio hai kama kuku na ng'ombe, walikuwa wakishuhudia kupitia televisheni tukio zima la sherehe ya uchumba ya Meryl na Mwisho.

Walikuwa wakiponda kila kitu kuanzia gauni alilovaa Meryl hadi mavazi ya washiriki waliobaki mjengoni ikiwa ni pamoja na hata wageni waliohudhuria.

KABLA YA SHEREHE

Wakati Uti na Munya wakivaa, Lerato alisikika akisema “Oh hapana! sio mvae ma-jeans…Munya anahitaji nguo mpya.” Lerato pia alisema shati la Uti halijampendeza.
Tatiana: Kuhusu gauni la Meryl; “Huwezi kuvaa gauni na viatu kama vile” na Lerato akaongeza; “Wanajaribu kufanya fasheni za karne ijayo.”

WAGENI WALIPOWASILI

Code: “Vichekesho vimeanza”
Lerato: “Mama yangu angeniua” “Familia wala haijafurahia (uchumba huu wa Mwisho na Meryl)”

Sheila: Wakati Munya akiendelea kuwahudumia wageni kwa vinywaji. “Hawataki kunywa, huoni? Wamestushwa (na uchumba huu)!”

Jen: Wakati Munya akikimbia mbele ya wageni. “Wakati nikitolewa mjengoni, jambo la kwanza nililotaka kufanya ni kumchapa kofi Munya.”
Tatiana: “Kwanini wameitwa mjomba na shangazi? Angalia upuuzi huu?”

KUVISHWA PETE

Paloma: “Oh Yesu wangu, Yesu wangu” huku mikoni ikiwa kichwani.
Jen: “Kuna taratibu kwa kila kabila, huwezi kuamka na kuamua kufunga ndoa.”
Lerato: “Ujue hawa wamechafua mzuka wangu wa kujirusha Jumamosi ya leo.”
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment