September 01, 2010

Kimwana Mkenya Sheila atupwa nje Big Brother

Wakati kimwana Mkenya Sheila, ametupwa nje ya Jumba la Big Brother, Tatiana ameeleza namna 'anavyomiss' boifrendi wake, jambo lililomfanya Yacob kumuuliza kimwana huyo wa Angola kama anadhani mwanaume Tatiana na Yacob walikuwa jikoni wakikata mboga wakati kimwana huyo alipoelezea namna 'anavyommisi' boifrendi wake. Yacob hakupoteza muda na akamuuuliza kama anadhani bado yuko na boifrendi wake huyo wa nje ya nyumba baada ya yote aliyoyafanya mjengoni.
wake huyo atakuwa anafurahia anayoyafanya ndani ya nyumba ya Big Brother.



Kimwana huyo tayari ameshabusiana na takriban kila mwanaume ndani ya jumba la Big Brother na baada ya kutolewa na kutupwa kwenye Zizi, amekuwa akifanya vitimbi kibao vya kimapenzi akiwa na kijana wa Uganda, Hannington. Yeye na Munya walioga pamoja mara kadhaa wakati wakiwa mjengoni na pia wakaambiana hata siri zao wakati wakiwa wamelala, jambo ambalo lilipelekea Munya kuadhibiwa kufuatia kumsimulia Tatiana hadi siri moja ambayo ni ya shindano.



Na sasa wakati akiwa ameshatupwa kwenye Zizi la Big Brother, Tatiana amekuwa akibusiana na kufanya kila wanaloweza kwa kila nafasi ndogo wanayoipata. Tatiana ambaye alivua nguo zote, alimpa Yacob pia shoo ya kuvua nguo katika usiku ambao Yacob aliwasili zizini kufuatia kutolewa kwenye Jumba la Big Brother.



Tatiana alimweleza Yacob kwamba boifrendi wake hajali chochote anachofanya ilimradi havuki mipaka. Alidai kuwa wao wanaaminia sana na kwamba siku akimchumbia, atakubali bila ya kusita. Yacob hakuficha jambo, akamweleza kwamba kama angekuwa yeye ndiye boifrendi wake, asingekubali mambo hayo.



"Kama mpenzi wangu atafanya hata nusu tu ya mambo haya unayoyafanya humu, nitapandwa na wazimu," alisema. Yacob aliendelea kusema kuwa ataachana mara moja na mwanamke wa aina hiyo, lakini akakiri kwamba pengine hafahamu jinsi Tatiana na boifrendi wake huyo walivyo huru katika mahusiano yao. "Watu wako tofauti," alisema Yacob.



Baadaye Yacob akaonyesha vituko baada ya kuwaonyesha memba wenzake wa zizini, Tatiana, Lerato na Hannington maeneo yake 'nyeti' ya mwili ambayo alisema yalinyolewa na kimwana wa Afrika Kusini, Lerato. Lerato alibaki akicheka huku akigongeana mikono na Tatiana, baada ya kijana huyo wa Ethiopia kuanika walichokifanya wakati wakiwa peke yao. Tatiana na Hannington walibaki wakiwa hawaamini wanachokiona baada ya Yacob kuwaonyesha maeneo hayo.



Sheila atupwa nje



Kimwana wa Kenya, Sheila, juzi Jumapili alikuwa mshiriki wa sita kutolewa kwenye Jumba la Big Brother, na kuacha simanzi na rafikiye mkubwa wa mjengoni, Uti, wa Nigeria. Huku akidhani kwamba anaonyeshwa njia ya kurejea nyumbani kwao Kenya, Sheila alijikuta akiingia zizini ambako alikutana na memba wenzake wote waliotolewa mjengoni, ukiacha Sammi wa Ghana, ambaye aliondoka mchezoni baada ya kuugua.



Usiku wakati wamelala, Sheila, alionekana akicheka na Lerato baada ya kuwasikia Tatiana na Hannington wakibuasiana kitandani usiku. Asubuhi, Sheila, alionekana ameshakuwa mwenyeji mapema baada ya kwenda kuanza kumkamua maziwa ng'ombe wao aitwaye Julliette.

No comments:

Post a Comment