Chegge Chigunda a.k.a Mtoto wa mama Saidi....wa TMK Wanaume Family amekiri hakuna wimbo wao uliowahi kuvuma kipindi kirefu kama "Mkono Mmoja" waliyofanya na Mh. Temba kwa kumshirikisha Wahu wa Kenya
. Lakini msanii huyo anakwenda mbali zaidi kwa kusisitiza kuwa muziki umebadilika kwani wasanii wa kweli wameanza kuonekana na wazushi wanaolazimisha vipaji wameanza kupotea kwenye bongo flava. "Mkono Mmoja' ni wimbo ambao umefanya vizuri Afrika Mashariki, umekaa kwenye chati tangu mwezi wa tatu mpaka sasa na bado unazidi kupeta watu wameukubali sana. "Ujumbe wake ni mwepesi na jinsi ulivyopangiliwa hauchoshi watu kusikiliza. "....umetuweka kwenye chati ya juu naweza kusema kila mahali unakubalika."
"Ukiangalia muziki umekuwa mgumu, sasa kila kukicha unaona mabadiliko ya kila aina, huyu yupo yule hayupo ndio mambo yanavyokuwa, watu wameelewa nani mkweli na nani anafoji."Wasanii wameanza kujichuja wenyewe, msanii wa ukweli anabaki kuwa wa ukweli, ambaye hajui anachokifanya anapotea. "Ndio maana umeona wale wanaoweza ndio wamebaki kuwa juu siku zote na ambao hawawezi wanaonekana hawawezi. Inaonekana wameshindwa ingawa siwezi kujua sababu nyingine zinazowakwamisha.
"Lakini kwa wenye akili wakiangalia wanaona ni wazi wanaojua wanachokifanya ndio wanapeta wengine wamechemsha. Huwezi kufoji kipaji kama huna huna...hujui hujui.." Msanii huyo anasema kuwa wamejipanga kutoka upya na singo ya 'Fungeni Milango' hivi karibuni ambayo wamefanya na Temba pia. "Tuna utaratibu wetu wa kazi tuliojiwekea kwamba sasa kwenye kundi ni zamu ya watu fulani kufanya kazi na muda fulani ni zamu ya watu fulani.
"Sasa ni zamu yangu na Temba ndio maana unaona kazi zetu ndiyo nyingi zimepewa nafasi, baada ya muda utasikia wengine na kundi hali kadhalika."Mfumo huo ndio tumekuwa tukitumia tangu awali na napenda kusisitiza kuwa kundi lipo imara kama kawaida na tutazidi kufanya vizuri kwa vile tuna ushirikiano wa dhati na kila mmoja ana uwezo na kile anachokifanya." Temba na Chegge ndiyo wamekuwa wakisikika katika siku za karibuni huku baadhi ya mashabiki wakihoji kulikoni kazi mpya za kundi zimekuwa hazisikiki.
No comments:
Post a Comment