September 04, 2010

Wahu a.k.a Mama Nameless Kuwapa Sweet Love Mamiss Tz

Wahu kutoka Kenya wanatarajiwa kupamba shindano la urembo la taifa mwaka huu 'Vodacom Miss Tanzania 2010' litakalofanyika Septemba 11 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga, alisema jana kuwa mbali na msanii huyo, pia kutakuwa na burudani nyingine kutoka kwa wasanii AY, Mheshimiwa Temba, Chege,THT na Mataluma.


Lundenga alisema kuwa warembo wote wanaendelea vizuri na maandalizi ya shindano hilo na leo watapanda jukwaani kwenye ukumbi wa Mbalamwezi kwa ajili ya kumsaka balozi wa Redd's. Alisema kuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo wako katika hatua za mwisho za kukamilisha zawadi za washindi na wakati wowote watazitangaza.

Warembo 30 wanaoshiriki shindano hilo, jana walipata nasaha kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Sanaa na Utamaduni nchini, Angella Ngowi, pamoja na Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Chiku Shomary.

Miriam Gerald kutoka Mwanza ndiye mrembo anayeshikilia taji hilo na yuko kambini na washiriki hao, akiwaandaa na shindano hilo ambalo mshindi ataiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia ya urembo.

No comments:

Post a Comment