August 23, 2010

Kibaka auawa kinyama, akatwa viungo na kuchomwa moto

WANANCHI wenye hasira alfajiri ya kuamkia leo walipambana na kundi la wahalifu katika barabara ya Kawawa palipo
na pori la magomeni na mkwajuni na kufanikiwa kumkamata mmoja na kumuua kisha kumchoma moto.

Tukio hilo la aina yake lililogusa hisia za wakazi wa magomeni na mkwajuni ambapo inadaiwa wahalifu hao walikua kundi la watu sita walimvamia mwendesha pikipiki aliyekua akikokota pikipiki hiyo majira ya alfajiri ambapo walimpora na kisha walimkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kupoteza fahamu.

Hata hivyo kwa hali isiyo ya kawaida wasamaria wema waliokuwa ndani ya daladala pamoja na wananchi wa jirani wakiwemo vijana waliokuwa wakifanya mazoezi karibu na eneo hilo na waumini waliokuwa wakitoka msikitini muda huo waliamua kupambana na kundi hilo ambapo walikimbia ndani ya msitu huo na kupotelea ng’ambo ya pili.

Wananachi walikimbizana nao wengine walipotea kimaajabu pasipo kuonekana hata hivyo mmoja wa wahalifu hao alizidiwa na kutiwa nguvuni na wananchi hao ambao waliamua kumshambulia ikiwemo kumng’oa meno kwa kutumia koleo,huku wengine wakimkatakata viganja na kwa kuvitenganisha tenganisha.

“Jamani tumesha choka kuleana sasa ni kuonyesha vitendo tunafanya tunachojua sisi’ alisikika mzee mmoja ambaye inadaiwa anafahamiana na mhanga aliyeporwa pikipiki.

Baada ya kuchukua dakika kadhaa, ambapo inadaiwa aliyeporwa pikipiki amekufa njiani akielekea Hospitali, wananchi hao walipandwa na hasira kali na walimvua nguo na kisha kumchoma moto na kufa huku akijiona.

Mwanablog wetu alifika eneo loa tukio muda mfupi na kukuta umati mkubwa ukiwa umejawa na simanzi kuona mwili wa mhalifu huyo ukiwa tayari umeshakakama.

Kifo cha mwizi huyo ni cha kusikitisha, kwani inadaiwa wananchi walimwagia mafuta sehemu za kichwani na tumboni ambapo walimzungushia mifuko ya pastiki na majani na moto huo uliweza kumuunguza eneo zima la juu mpaka kupelekea utumbo kupasuka ndipo walipoondoka na kumuacha katikati ya uwanja wa Kinondoni Mosco na Magomeni Suna. Baadhi ya wananchi waliongea Mwanahabari wetu juu ya tukio hilo walidai kuwa wamesha choka na vitendo vinavyo fanywa na wahalifu hao kwani walishalalamika muda mrefu juu ya kuondolewa msitu huo.“Tunamtaka Mkuu wa Wilaya atuambie ukweli kama huu msitu wameupanda kupoteza watu ama wameupanda kwa lengo gani!!.. maana hauna manufaa yoyote kwa wananchi kila siku tunashuhudia uhalifu’ alisema Zainabu mkazi wa Kinondoni Mosco.

Kwa upande wake Shahibu Hussein ambaye alishuhudia tukio hilo alidai kuwa ndani ya miezi miwili wamesha kufa watu watatu, aidha inadaiwa tokea kushamiri kwa msitu huo tayari zilishaokotwa maiti nne zikiwa zimeharibiwa vibaya na wahalifu.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Peter Kalinga alisema kuwa hayupo ofisini ila atalishughulikia kwa kukusanya taarifa kwa watendaji wake na kulitolea ufumbuzi swala hilo .

“Nipo katika kikao, ngoja nilifuatilie nitakupa majibu’ alisema Kalinga kwa njia ya simu.

Wananchi hao wameapa na kutangaaza vita kali kwa kujichukulia hatua za haraka ikiwemo kuwaua wahalifu ambao wanatumia msitu huo kama ngome yao ikiwemo na hatua ya kupeleka viwiliwili kwa ofisi ya mkuu wa Wilaya.

‘Kilichobaki, Mbunge,diwani na Mkuu wa Wilaya wameshindwa kulitolea ufumbuzi swala hili hivyo tunahakikisha kila atakayepatikana ndani ya msitu huu kwa kosa la uhalifu ni kutenganishwa kisha viwiliwili tunawapelekea huko huko ofisini kwao tumechoka tunataka haki yetu’ walisikika vijana waliokuwa wamejaa na hasira.

Source: MO Blog



No comments:

Post a Comment