September 05, 2010

Vodacom Miss Tanzania 2010 kujizolea Milioni 46.6

 

Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akitangaza rasmi zawadi za zitakazotolewa kwa washindi katika shindano la Vodacom Miss Tanzania litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam septemba 11 jumamosi. Akizungumzia zawadi hizo amesema jumla ya shilingi milioni 46.6 na gari aina ya Hyundai i10 lenye thamani ya shilingi milioni 12, Amesema mrembo huyo pia atajipatia shilingi milioni 10 fedha taslimu pamoja na kujishindia zawadi ya gari. Mshindi wa pili atajipatia shinilingi milioni 6.2 wakati mshindi wa tatu atajipatia shilingi milioni 4, mshindi wa tatu atajipatia shilingi milioni 3, mshindi wa nne atapata shilingi milioni 2.4 na wa tano atapata shilingi milioni 1.4 huku washiriki wengine wakipata kifuta jasho cha shilingi laki 700.000


 
Mkuu wa Udhamini wa Voodacom Miss Tanzania George Rwehumbiza akisaidiana na warembo kufunua gari la zawadi ya mshindi wa shindano hilo wakati wa kutangaza zawadi za zitakazotolewa na Kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyoko ufukweni wa bahari ya Hindi huko Mbezi Beach.


Warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakifurahia gari litakalotolewa kama zawadi katika shindano hilo. 

 

Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza mwenye kofia Mkuu wa Itifaki Miss Tanzania Albert Makoye wakipiga picha pamoja na warembo mara baada ya kuonyeshwa gari aina ya Hyundai i10 litakalotolewa kama zawadi kwa mshindi wa shindano hilo. 

Sorce: Dullonet
 




No comments:

Post a Comment