September 05, 2010

20 Za Town Kutoka Kwa TV Host CASTO Comin' Soon Ndani Ya Clouds TV.

Anaitwa Casto kijana kutoka Clouds TV na hapa alikuwa akifanya Interview ya kipindi chake kipya ambacho kitazinduliwa soon na kitatambulika kwa jina la 20 za Town ambacho kitakuwa kikirushwa kila Jumamosi usiku Clouds TV. Kipindi hiki kitakuwa kinazungumzia Bongo Flava pamoja na videos za bongo na bila kusahau Interview kwa wadau wote wa mziki huu wa bongo fleva.

Alianza na Dj Maarufu Mjini (Dj Choka Kutoka Bongo Star Link) Mr. Apetite Alipigwa Maswali  tofauti tofauti juu ya blog yake na mambo mengine mengi ambayo majibu yake yalikuwa mepesi kuyajibu. Location hii ilikuwa pale Mlimani City. 
  
 
Baada ya hapo Crew Nzima Ya Clouds TV Ikaelekea kwa msanii Young D kutoka Fish Crab naye alikuwa akiulizwa maswali ya kimuziki zaidi pamoja na stylez  anazofanya kama yeye anauchukuliaje Muziki wa Bongo kwa miaka ya baadae. Location hii ilikuwa pale Ubungo Plaza.

 
 Show ya Casto ikaishika kwa msanii mwingine anayejulikana kwa jina la CPWAA, huyu yeye alikuwa akiulizwa juu ya video mpya aliyoitoa ambayo inaitwa So Pwaa. . Location ilikuwa pale Mbalamwezi Beach.
 c
Vijana kutoka mjengoni Clouds TV hawa hapa, Casto a.k.a (Mwananchi Wa Kawaida), Raymond & Joram

Source: Bongo Star Link
 


No comments:

Post a Comment