September 11, 2010

H-baba atambulisha za hatari!

Mkali wa miondoko ya TAKEU Bongo, Hamisi Baba a.k.a H- Baba, ameibuka na kutambulisha staili mpya ya muziki, ambayo amesema anaamini itafunika ile mbaya na kumfanya aendelee kuwa kileleni. H Baba, alitambulisha style hiyo last week kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na Kituo cha Runinga cha EATV kila Ijumaa, ambapo aliitaja kwa jina la Poteza Dansi Bongo Fleva.

“Hapa watu watanikoma, maana haiigiki mzazi...ni mauno mwanzo mwisho, nani ataweza? Watu wasubiri kidogo waone ujio wangu mpya,” alisema H Baba.
 

No comments:

Post a Comment