September 11, 2010

Miss Tanzania 2010 leo ndio leo

Warembo wa Miss Tanzania 2010 wakiangalia gari aina ya Hyundai i10 atakalopewa mshindi wa kwanza katika shindano lao litakalofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Mwisho ya maswali ya nani atakuwa mrembo wa mwaka huu ni leo wakati vimwana 30 watakapopanda stejini kwenye Ukumbi wa Mlimani City kutafuta mshindi wa taji la Vodacom Miss Tanzania 2010.


Kwa mujibu wa Hashim Lundenga, mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency iliyoandaa mashindano hayo makubwa zaidi ya fani ya urembo nchini, wasanii mbalimbali watatumbuiza kuipamba shughuli yenyewe.

Wasanii watakaotumbuiza katika mashindano hayo, ni Wahu kutoka nchini Kenya, AY, Mheshimiwa Temba, Chege, Diamond, Lina, Barnaba, na bendi ya Tanzanite.

Mshindi wa kwanza katika mashindano ya leo ataondoka na gari ndogo aina ya Hyundai i10 yenye thamani ya Sh. Milioni 10, pamoja, fedha taslimu Sh. Milioni 10 na tiketi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss World.

Hadi sasa, Miss Tanzania aliyefanya vyema zaidi katika mashindano hayo ya dunia ni Nancy Sumari kwa kutwaa taji la Miss World Africa 2005.

No comments:

Post a Comment