October 11, 2010

Tinie Tempah Hawezi Kuandika Ngoma Zake Bila BlackBerry:

 
The 'Pass Out' hitmaker Mwenye Asili Ya Nigeria But Kikazi Zaidi Yuko kwa Kwa Mjomba Obama amekiri kuwa amekuwa addicted na Teknolojia Ya kisasa katika simu yake aina ya blackberry ambayo huitumia katika kuandika mambo yake kibao ikiwemo mistari mikali mfano ni ngoma kali zilizomo katika mixtape yake ya Discovery Iliyoko Online Kwa Ajili Ya Mashabiki Wake, Na Mara Nyingi Amekuwa Akiitumia Simu Yake Hiyo Anapokua Katika Tour Mbalimbali.

Tempah Anasema: ' Hajapanga ni muda gani wa kuandika mistari au kuimba, huwa anaandika akiwa popote na muda wowote. Huwa anaibeba blackberry yake na akipata idea yoyote anaiandikia note au kuirekodi katika simu yake na kila mwisho wa wiki anakuwa amepata zaidi ya sauti 40 kisha kuziandikia Lyrics zake au kuziunganisha kwa pamoja.

Kila Mara anakuwa bizy kuandika project mpya kwasababu hana muda maalumu alioutenga kwa ajili ya kaundika mistari yake.

Rapa Huyo wa Kibao cha Invicible ameeleza kuwa anathamini sana teknolojia ya sasa ambapo watu wamekuwa wakinunua muziki kupitia mitandao ya internet hali ambayo hata kwake imempa mafanikio makubwa aliyonayo sasa.

Tinie Tempah Ameingia Katika Orodha Ya Wasanii 100 Bora waliofanikiwa kutoka kimuziki kupitia katika huduma ya mitandao ya internet.

No comments:

Post a Comment