October 12, 2010

Maisha Halisi Na Muziki Kuhusu Mfalme Wa Mtindo Wa Kurap Fasta Twista Kuwekwa Katika Documentary:

Mr. Immortality: The Life and Times of Twista, Ni Jina La Filamu mpya ya Rapa Twista Kutoka St. Louis iliyoongozwa na Vlad Yudin, Kama jina lake linavyosomeka filamu hii itahusu kila kitu kuhusu maisha ya kawaida na kimuziki ya msanii huyu. Filamu hii itaingia sokoni mnamo tarehe 7 December Mwaka huu ikiwa chini ya usimamizi wa kampuni ya EMI.

Katika Muvi hiyo zitaoneshwa kila aina ya maisha aliyopitia Rapa huyo, sehemu aliyozaliwa,kukulia na mambo mengine kibao. Na Wageni waalikwa katika filamu hiyo ni pamoja na The Dream, Ne-Yo, Produza Scott Storch na wengineo pia kutakuwa na scene zitakazomuonesha akifanya kazi na Wasanii kama Jay Z na Kanye West.

Kabla ya Kuingia Sokoni kwa Filamu hiyo, Twista pia anajiandaa kuachia albamu yake iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya "The Perfect Storm" ambayo itaingia sokoni mwezi November tarehe 9 ikiwa chini ya Lebo za EMI/Capitol Records.

No comments:

Post a Comment