October 14, 2010

Albamu Ya Iveta Inakimbiza Vibaya Sokoni:

Album yenye jina la IVETA ya kwake msanii SAJNA kutoka pande za Rock City inaendelea kukimbiza sokoni ikiwa na ngoma za kijanja zipatazo kumi. Kwa mujibu wa meneja wa 'dogo' huyo, Kid Bwoy ambaye ametoka hospitalini Bugando, Mwanza hivi karibuni alikokuwa amelazwa, albamu hiyo ambayo iliingia kitaani siku kadhaa zilizopita inaendelea kufanya vyema sokoni na kuleta mapinduzi ya mauzo.

Albam hiyo ambayo ilianza kutengenezwa Januari, 2010 na kukamilika Julai, 2010 imewashirikisha wasanii wengine kama Belle 9, Linah wa THT, Josefly kutoka Musoma, Mara pamoja na Pipi.

Kid anasema ngoma itakayofuata baada ya Iveta itategemea na maoni ya wadau kwakuwa zote ni kali, japo amezitaja mbili ambazo ni Sitaki Kuumizwa iliyomshirikisha Linah na Roho Mbaya iliyowapa shavu Belle 9 na Pipi zitakazopigiwa kura.

No comments:

Post a Comment