October 12, 2010

Cassidy azungumza na maDj kuhusu Maandalizi ya "C.A.S.H" Na Mahusiano Yake Na Produza Swizz Beatz Baada Ya Kuachana Na Mkataba Wa Muda Mrefu Na Lebo Ya J Records:

Rapa Cassidy ametoa maelezo haya kupitia mtandao wa habari za wasanii uitwao TakeThisSerious.com, akielezea kuhusu ujio wa albam yake mpya ya nne inayosubiriwa toka kitambo ya "C.A.S.H. (Cass Always Stays Hard) na hakusita pia kuelezea mahusiano yake na produza aliemtoa kimuziki Swizz Beatz aliyepata kutengeneza ngoma kali zilizowahi kufanya vizuri kama "Hotel, I'm a Hustla na My Drink N My 2 Step," na nyinginezo kibao.

The Philly Emcee Amesema kwamba japokuwa Cassidy hajasaini makataba na Swizz na badala yake amesaini contract na "Carmelo Anthony's Kross Over Entertainment in '09), Still ana mahusiano mazuri na Prodyuza huyo na anafuraha kuwa huru kupanga maisha yake ya badaye kama msanii.

"Sipo katika mkataba wa muda mrefu tena, lakini bado nina uhusiano mzuri na Swizz. Hatuwasiliani kila siku ila tunaongea kila mara. Beatz ni mtu kazi a.k.a buzy man, anafanya mambo yake kwa sasa, siko studio kila mara kama zamani but kila kitu kanatokea kwa sababu maalumu. Nina furaha kupata kampuni yenye uwezo wa kumfanya msanii awe juu kama nilivyokuwa kwa Swizz Beatz.....So imekuwa vizuri jamaa ameamua kufocus mambo yake yakibiashara na familia yake kama ilivyo kwangu. Wote Tunatakiwa kufight ili kupata chochote mezani na kuingiza pesa pia, nimejifunza mengi kuwa karibu na Swizz, Daima nitamheshimu Swizz na kumpenda.

Na Alipoulizwa kuhusu Kuhusika kwa Swizz Katika ujio wa Long Play CD Yake mpya, amejibu kuwa hawezi kuzungumza kwa sasa but ngoma nyingi zilizomo katika albam yake ya CASH Zimefanywa na Swizz ikiwemo ngoma aliyomshirikisha John Legend iitwayo "Searchin":

No comments:

Post a Comment