November 27, 2011

Wanajeshi Wa Misri Wanyoosha Mikono Juu!!

Stori kutoka Misri, zinaamplfy kwamba  baada ya mizengwe kuzidi, Watawala wa kijeshi wa nchi hiyo wamemteua waziri mkuu wa zamani Kamal Ganzouri kuunda serikali mpya huku Baraza la mawaziri la kiraia lilokuwa limeteuliwa na jeshi,


lilijiuzulu wiki hii wakati maandamano yalipoanza kwenye miji mbalimbali ya nchi hiyo ambapo sasa hivi Baraza la kijeshi limesema uchaguzi wa wabunge utaanza wiki ijayo kote nchini humo.

Vurugu za karibu na medani ya Tahrir yamepungua ambapo mpaka sasa Idadi kubwa ya waandamanaji wanalala katika medani ya Tahrir wakijiandaa kwa mkutano mkubwa siku ya Ijumaa ambapo Baraza kuu linalotawala la kijeshi linasimamia mpango wa mabadiliko hadi katika utawala wa kiraia kufuatia kupinduliwa kwa Rais Hosni Mubarak mwezi Februari.

Licha ya ahadi za baraza hilo kuharakisha mchakato wa mabadiliko, raia wengi wa Misri wanaogopa kuwa jeshi lina nia ya kuendelea kubaki madarakani, Ganzouri aliongoza serikali ya Misri kutoka mwaka 1996 hadi mwaka 1999 chini ya utawala wa Bwana Mubarak na Gazeti la serikali al-Ahram limeandika kwamba Bwana Ganzouri amekubali kuongoza serikali baada ya kukutana na kiongozi wa baraza la kijeshi Mohamed Hussein Tantawi.

No comments:

Post a Comment