November 27, 2011

Muvi Ya "CPU" Yaoneshwa Kwa Mara Kwanza Ndani Ya Mlimani City Bongo Cinema


Movie ya CPU ambayo kama sijakosea itakua ni movie ya kwanza ya kibongo maandalizi yake na mpaka movie kukamilika yamechukua muda mrefu, imeonyeshwa kwenye BIG SCREEN ya ukumbi wa CINEMA mkubwa kuliko yote Tanzania, Mlimani CITY.

movie hiyo iliyoandaliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, itaonyeshwa kwa zaidi ya siku sita pale Mlimani city kama zinavyoonyeshwa movie nyingine za nje ya Bongo, maandalizi ya kuitengeneza yalianza toka mwaka jana, mwandishi wa script ni Novatus ambae alikua akiishi Uingereza, na Producer mkubwa ni Martin Muhando, muhadhiri wa chuo kikuu cha AUSTRALIA.

sio movie ya ACTION, stori yake ni kipelelezi kuhusu haki za watoto wanaoingia mtaani lakini hakuna anaefaham chanzo chake, kabla ya kuanza kuwakusanya watoto na kuwaweka pamoja, CPU inatafuta nini chanzo, sasa jinsi ilivyoigizwa kiteknolojia ndio utapenda amesema Myovella mfwaisa, mmoja kati ya waandaaji.

CPU ilichozwa DAR ES SALAAM katika location 32 tofauti nyingine zikiwa zimepigwa kwa kutumia HELCOPTER, ni movie ambayo asilimia kubwa ya picha zake, zilipigwa kutoka angani kwa kutumia helkopta iliyokodiwa, na mitambo ya kisasa kama wanayotumia watengenezaji wa movie marekani na nchi nyingine zilizoendelea.

Ni movie ambayo bajeti yake inatajwa kuwa kubwa lakini inalingana na ubora, ambapo waandaaji wataweka hadharani siku chache zijazo.

No comments:

Post a Comment