November 27, 2011

Producer Man Walter Kutoka Combination Sound Asistiza Kutomsamehe 20%



Baada ya MAN WATER ambae ni producer wa msanii 20% kuongea ukweli siku tatu zilizopita kwenye AMPLIFAYA, kwamba yeye na 20% hawapatani na hawajawasiliana kwa zaidi ya miezi sita,
leo amezungumzia kuhusu kumsamehe.

Chanzo cha wao kugombana, ugomvi ambao ulifanywa siri kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari hadi juzi alipofunguka EXCLUSIVE kwenye amplifaya, ni 20% kudaiwa kutaka kumpiga producer huyo kwa kutaka alipwe pesa ya show yake iliyofanyika Morogoro.

ishu ilikua ndogo tu, Man water alimwambia subiri nimalizie kufungua vyombo kwenye stage ili nikakupe hela shilingi laki nne iko kwenye gari, lakini 20 alikataa akaanza kutoa maneno ya kashfa.

Man water ambae ndio producer wa nyimbo mbili zilizompa 20% tuzo tano za KTMA mwaka huu, amedai kuna maneno mengi mabaya ambayo 20% aliyasema siku hiyo mbali na kumkunja shati kutaka kumpiga producer huyo…. “alisema mimi ni producer gani, studio ziko nyingi tu, na hatokanyaga tena kwenye hii studio, na atanifanyia kitu ambacho sitosahau kwenye maisha yangu, ni kauli nzito sana ningeweza kumshitaki lakini nimeamua kutulia nisubirie kama ataniua au vipi, MIMI NI MKRISTO nafahamu kuna kusamehe, ila kwake siwezi, SIWEZI KUMSAMEHE kwa sababu alinidhalilisha sana, SIWEZI” ameamplfy MAN WATER
japokua man water amesema hawezi kumsamehe, 20% juzi pamoja na kwamba alikiri ugomvi kutokea, alisema anaamini ataendelea kufanya kazi na man water katika siku zijazo.

No comments:

Post a Comment