November 30, 2011

Linnah Amtosa Mwana FA Kwenye Show Ya St8rt Muzik

MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Estalina Sanga ‘Linah’ (pichani) juzikati ndani ya Viwanja vya Leaders Club jijini Dar ‘alimtosa’ msanii mwenzake, Khamis Mwinyijuma ‘MwanaFA’ baada ya kugoma kupanda jukwaani kuimba naye wimbo wa Yalaiti aliomshirikisha.

Kitendo hicho kilitokea kiwanjani hapo kulipokuwa na Tamasha la Inter-Collage lililoandaliwa na Str8muzik na kuwashangaza wadau waliokuwa wakitegemea kumuona Linah akimpa sapoti MwanaFA.
Linah alipoulizwa sababu ya kushindwa kupanda jukwaani, hakujibu chochote zaidi ya kuangalia pembeni kana kwamba alikuwa hasikii  kile alichoulizwa na paparazi wetu.

No comments:

Post a Comment