November 27, 2011

Ben Pol Ashawishiwa Kujiunga Na FREEMASONS Ili Afanikiwe.

Mara nyingi tumezoea kusikia shutuma kuhusu stori za mastaa wa dunia hata marais wa nchi kuwa waumini wa dini inayomuabudu shetani, kama marais kadhaa wa marekani akiwemo George Bush,
na mastaa wengine kama Jay z, Beyonce, Rick Ross, Lil wyne na wengine.

Lakini sasa leo stori inatoka bongo dar es salaam ambapo mwimbaji BEN POL, ambae usiku wa leo aliota ndoto ya kutisha akiwa hajawah kuiota katika maisha yake, ambapo leo aliandika kwenye faceBook kwamba “kanisa linalomuabudu shetani limenilazimisha nijiunge nalo, NI SAA 8 NA DAKIKA 3 USIKU ..NIMEOTA NDOTO YA AJABU..nilikua naongea na shetani na nikamwambia straight, sitaki..,SIwezi kuwa muumini wa kanisa hilo …MWILI UNATETEMEKA HAPA NAANDIKA HII STATUS” ameandika BEN POL 

Japo amekua akiota ndoto nyingi, anasema asilimia kubwa hazijawah kumtokea kwenye maisha yake, lakini bado yuko njia panda kwa sababu hajaelewa kama huwa zinamtokea kweli ila anashindwa kufaham kutokana na kukosa TAFSIRI ya ndoto yenyewe.

Hata hivyo kwa sasa anafikiri kwenda kanisani kwa ajili ya kuombewa ili Mungu amuepushe na mialiko hiyo miwili ya kujiunga na dini ya kishetani. 

akiamplfy EXCLUSIVE kwenye millardayo.com BEN amesema ndoto ya leo ni mwaliko wa kwanza wa kujiunga na dini hiyo, ila alishawah kupata mwaliko mwingine kwenye ukurasa wake wa facebook japo hakuwah kutangaza, aliuIGNORE.

No comments:

Post a Comment